Tarehe May 15, 2015
Msanii wa muziki nchini Tanzania, Vanessa Mdee amekiri kuachana na utangazaji na kuwekeza nguvu zake katika muziki ikiwa ni jibu ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki wake baada ya kuulizwa sana swali hilo.
Amesema kuwa kutokana na kasi ya ukuaji wa muziki hana budi kuachana na utangazaji na kujikita katika muziki kwani muziki unahitaji muda na utulivu ili kuweza kufanya vizuri.
Ameendelea kufunguka zaidi kuwa kwa sasa ana shoo nyingi nje ya Dar es Salaam na kutengeneza video nyingi nje ya nchi, hivyo aliona ni bora kuachana na utangazaji ili asiwakwaze wakubwa wake wa kazi.
Post a Comment