STAA wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel ‘mama Cookie’ amewajia juu wanaomsema kuwa amekikacha Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kukimbilia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa hajazaliwa na chama hicho bali amezaliwa Kisarawe.
Aunt amesema kuwa hata kama huko alipo wakishindwa atakubali matokeo kwa kuwa lazima katika mchezo kuna upande utashinda na mwingine utashindwa hivyo atakubali yote.
“Ninachojua mwisho wa siku lazima kuna mshindi na mshindwa hivyo nakubali yote kwa sababu nampenda Lowassa na sijawahi kutamka kuwa mimi ni CCM kwa kuwa sijazaliwa kwenye chama hicho, nimezaliwa kijijini kwetu Kisarawe "alisema Aunt kwa jazba.
Post a Comment