Tatizo La Kuwahi Kufika Kileleni Ni Nini?
Kuwahi kufika kileleni au kuwahi kumaliza tendo la ndoa au kwa lugha ya mtaani kukojoa upesi ni hali ambayo inampata mwanamme ambapo hutoa shahawa kabla ya kuanza tendo la ndoa au muda mfupi tu baada ya kuanza tendo bila yeye mwenyewe kukusudia . Kwa kawaida mtu mwenye tatizo hili hutoa mbegu zake za kiume hata baada ya maandalizi kidogo sana. Tatizo hili hujidhihirisha zaidi kwa vijana wenye umri mdogo na hupungua kadri umri wa mtu unavyoongezeka. Karibu kila mwanamme kwa wakati fulani hupata tatizo hili lakini baadhi ya wanaume wenye umri wa kati huwa na tatizo la kudumu. Kwa bahati nzuri tatizo hili limepatiwa ufumbuzi na tiba inapatikana.
Chanzo Cha Tatizo La Kuwahi Kufika Kileleni
Chanzo kamili cha tatizo hili bado hakijafahamika. Lakini imethibika kwamba wasiwasi au mishipa ya fahamu inahusika sana na tatizo hili. Hali hii inaweza kutokea unapompata mpenzi mpya au unapofanya tendo hili baada ya muda mrefu kupita toka ulipotoa shahawa mara ya mwisho. Hii ndiyo sababu iliyofanya baadhi ya wanaume kugundua kuwa wakinywa pombe kidogo, huwapunguzia wasiwasi na huwasaidia wachelewe kufika kileleni. Mara nyingine tatizo hili linatokana na matatizo katika mfumo wa homoni za mtu au likiwa ni matokeo ya matumizi baadhi ya madawa.
Tiba Ya Tatizo La Kuwahi Kufika Kileleni
Kwa kawaida tatizo la kuwahi kufika kileleni mapema ni tatizo ambalo huondoka lenyewe kadri umri unavyokuwa unasogea mbele. Kama tatizo sio kubwa sana, kwa mfano, kama unamudu kuendelea na tendo la ndoa kwa dakika tano na ungependa kufikisha dakika kumi, wewe sio mtu wa kumwona daktari bali mtu ambaye unaweza kufanya mazoezi fulani ya kuongeza muda wako. Vitu rahisi vya kufanya ni kutokuwa na papara, kutulia na kondoa mawazo yako kutoka kwenye tendo na kuyapeleka mbali kwenye jambo jingine tofauti kabisa unapokaribia kufika kileleni. Unaweza kufanya utafiti na mpenzi wako mkapata mtindo (sexual position) ambao utakusaidia usifike kileleni mapema. Kama hali yako ni mbaya zaidi, unaweza kutumia njia zifuatazo:
1. Kufanya mazoezi yanayosaidia kuondoa tatizo la kuwahi kufika kileleni. Hapa chini ni orodha ya baadhi ya mazoezi unayoweza kufanya;
- Kuvuta Na Kutoa Pumzi (Deep Breathing)
- Kuanza Na Kukatisha (The Stop-and-Start Method)
- Kuminya (The Squeeze Method)
- Mazoezi Ya Kegel (Kegel Exercises)
- Mazoezi Ya Tantra (Tantric Techniques)
Mazoezi ya Kegel tumeyapata umuhimu wa kipekee kutokana na ubora wake katika kuondoa tatizo la kukojoa upesi na tumeandika ukurasa wa pekee kwa mazoezi hayo. Katika ukurasa huo tumeweka video moja ya kuonyesha jinsi ya kufanya mazoezi hayo.
2. Kutumia kondomu maalumu (Condoms With Benzocaine). Kondomu hizi hukusaidia uendelee na tendo la ndoa na kuongeza muda wako wa kufika kileleni kwa kiwango cha hadi dakika tano. Kondomu hizi huwekwa benzocaine ambayo hutia ganzi kwa kiwango kidogo sehemu ya kichwa ya uume ili kupunguza usikivu wa nyege (sexual sensation) na kumfanya mwanamme aweze kutawala muda wake wa kufika kileleni.
3. Kutumia dawa zilizotengenezwa mahsusi kwa tatizo hili (Antidepressant medicines). Dawa ambazo zimekuwa zikitumika ni pamoja na clomipramine (Anafranil) na dapoxetine (Priligy). Tramadol (Ultram), dawa ambayo hutumika kuondoa maumivu, hutumika pia kuondoa tatizo hili.
Kuna creams, gels na sprays ambazo zimetengenezwa kupambana na tatizo la kukojoa haraka. Hizi hufanya kazi kwa kupunguza usikivu wa nyege kwenye dhakari. Mfano wa dawa hizi ni lidocaine au lidocaine-prilocaine ambayo hupakwa kwenye uume kabla ya kuanza kujamiiana.
Katika mada nyingine tutalizungumzia tatizo ambalo linasumbua watu wengi sana katika jamii yetu, nalo ni tatizo la jogoo kushindwa kuwika (Erectile dysfunction) au kwa lugha ya mitaani tatizo la uume kushindwa kusimama.
Post a Comment