LEO tunaelezea madhara ya kitambi na tutafafanua jinsi mafuta yanavyozidi mwilini na kuathiri ini pia tutaeleza tiba yake, endelea:
Utambuzi wa steatosisi hufanywa wakati mafuta yaliyo kwenye ini yanazidi asilimia 5 hadi 10 kwa uzito.
Kuwa na mafuta kwenye ini ni tatizo au linaweza kuchukuliwa kama ugonjwa mmoja ambao hutokea kwa wale hasa wanaokunywa pombe kupita kiasi.
Kuwa na mafuta kwenye ini ni tatizo au linaweza kuchukuliwa kama ugonjwa mmoja ambao hutokea kwa wale hasa wanaokunywa pombe kupita kiasi.
Tatizo hili licha ya kusababisha unene pia linahusishwa na magonjwa mengine ambayo huathiri umetaboli wa mafuta.Kimofolojia, ni vigumu kutofautisha kati ya FLD inayohusishwa na pombe na ile isiyohusishwa na pombe na aina zote mbili huonyesha mabadiliko ya vilengelenge vidogo na vikubwa vya mafuta katika hatua mbalimbali.
Tatizo hili la mafuta kukusanyika kwenye ini kunaweza kukasababisha kuvimba kwa ini (hepataitisi), tatizo liitwalo kitaalamu steatohepataitisi.Kwa kuzingatia mchango na pombe, ukusanyikaji wa mafuta kwenye ini unaweza kuitwa steatosisi ya pombe au ugonjwa wa ini kuwa na mafuta usiohusiana na pombe (NAFLD).
Licha ya unene kupindukia kusababisha mafuta kujaa kwenye ini, ukusanyikaji wa mafuta kwenye sehemu hiyo (ini) huhusishwa na pombe au tatizo la ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu.Lakini pia sababu za lishe kama vile utapiamlo, kupoteza uzito sana, matatizo yanayotokana na kula baada ya kukaa kwa muda mrefu bila chakula, ukwepaji wa ufyonzaji wa chakula katika matumbo, ni sababu nyingine za ugonjwa huu.
Ini lililovimba sana na lenye kiwango cha juu cha steatosisi mara nyingi huendelea hadi kwenye aina kali zaidi ya ugonjwa huu.Tiba na ushauriMatibabu ya mtu aliye na mafuta kwenye ini yanategemea na kilichosababisha athari hiyo.
Watu waepuke kunywa pombe kupita kiasi japokuwa matukio ya saratani ya ini katika FLD isiyosababishwa na pombe bado hayajahesabiwa, lakini uhusiano uliopo ni dhahiri kwamba ni tatizo.Asilimia 75 ya watu walio na unene wa kupindukia hukumbwa na tatizo hili ingawa hakuna ushahidi wa matumizi ya pombe kupita kiasi kwamba kunasababisha maradhi haya
Post a Comment