Jennifer Kyaka a.k.a Odama ni msanii ambaye anafanya poa kwenye Tasnia ya filamu hapa Tanzania ikiwa hata jina la ‘Odama’ limetokana na jina la Filamu inayoitwa ‘Odama’ Filamu ambayo ndio iliyomtambulisha. Hivyo basi kutokana na faida ambazo ‘Odama’ anazipata kupitia sanaa ya uigizaji imesababisha awaweke wazi wanaume ambao wanamnyemelea kumuoa ili baadaye isije ikawa shida kwenye ndoa kama ilivyo kwenye ndoa zingine. siku za hivi karibuni Odama alifunguka kwenye chanzo chetu kuhusiana na issue hii.
“Kwa yule ambaye atakuja kuwania kunioa, kwanza lazima atambue kuwa nafanya filamu, sitahitaji anieleze jambo la kuacha kazi yangu, mimi ni mwanamke ambaye nahitaji kupata maendeleo kupitia kazi yangu ambayo imenitoa mbali hivyo siwezi kuiacha”
Post a Comment