Leo tutagusia matibabu ya tatizo hilo ambalo linawakabili karibu asilimia 30 ya wanaume duniani huku kati yao asilimia 8 hadi 10 wakiwa katika maeneo tofauti duniani. Imegundulika kwamba, ugumba hutokea zaidi maeneo ambayo jamii ina uwezo mkubwa zaidi wa kuzaliana (barrenness amid plenty).
Sehemu ya matibabu ya ugumba kwa mwanaume ni pamoja na wanandoa au wenzi kuungana pamoja kutafuta matibabu, hapo uhitaji kupatiwa elimu ya kutosha juu ya tatizo. Siyo busara mmoja kumnyanyapaa mwenzake au kumtenga, bali kumpa ushirikiano. Iwapo tatizo limegundulika kuwa limetoka na mfumo mbovu wa maisha, mfano; kuvuta sigara au kunywa pombe kupindukia, basi mgonjwa huaswa kubadili mfumo huo wa maisha. Mwanaume kufanya mazoezi kupita kiasi, unene uliopindukia, kuvaa nguo za ndani zenye joto pia hutakiwa kuepukwa. Haya husaidia kuboresha mbegu za kiume na kuziwezesha kumtungisha mimba mwanamke, hivyo kukwepa dawa ama upasuaji.
Iwapo mirija ya kupitisha mbegu za uzazi itakuwa imeziba na imethibishwa kwa vipimo, basi upasuaji hufanyika kuzibua mirija hiyo. Kama mirija ya damu katika korodani au njia ya kuu ya kupitisha mbegu imekuwa mikubwa kupita kiasi,kuyumba na kusababisha joto, basi upasuaji hufanyika pia kurekebisha tatizo hilo.
Dawa zipo, lakini hutolewa iwapo mgonjwa amethibitika kuwa na tatizo katika homoni zake na hivyo kusababisha uzalishaji mdogo wa mbegu au kutozalisha kabisa kwani matatizo ya homini za uzazi kwa mwanaume pia huchangia kuleta ugumba. Ikumbukwe kwamba maambukizi katika mfumo wa uzazi na kukojoa, huchangia kuleta ugumba. Iwapo hili limegundulika, mgonjwa hupewa dawa kwa ajili ya kuua vijidudu vya maambukizi, hivyo kuboresha mbegu.
Njia nyingine ya kitaalamu na kisasa, ni mgonjwa mwenye ugumba kuweza kufanyiwa upasuaji mdogo wa kunyonya au kuvuta mbegu za kiume kutumia chombo maalumu kutoka katika korodani, kisha kuzipandikiza kwa mwanamke, pale kipimo cha kukata nyama kinapoonyesha mbegu zipo safi lakini ni chache au njia mbadala hapo juu zimeshindikana. Matibabu haya yana gharama kidogo, lakini yamesaidia wanandoa wengi kupata watoto.
Post a Comment