MKALI WA MAIGIZO YA KUCHEKESHA BONGO,DICKSON SAMSON MAKWAYA A,.K.A BAMBO ALFAJIRI YA LEO AMEPATA AJALI MBAYA YA PIKIPIKI NA KUVUNJIKA MGUU WAKE WAKULIA
NA PIA KATIKA SEHEMU YAKE YA JUU YA PAJA IMEJERUHIWA VIBAYA NA KUUNGUZWA NA BOMBA LAKUTOLEA MOSHI LA PIKIPIKI
Wasanii wenzake na Bambo wakiwa na sura za majonzi mara walipofika hospitalini kumwona mwenzao Dickson Samson Makwaya a.k.a Bambo aliyelazwa kitandani. Picha inayofuata ni dereva wa pikipiki waliyopata nayo ajali alfajiri ya leo.
. Dereva wa pikipiki aitwae Jumbe Juma kwa sasa hali yake ni mbaya na wote wamelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.
Bambo aliyejitwalia umaarufu mkubwa miaka ya 90 akiwa na Kundi la Sanaa la Kaole ambalo lilikuwa likirusha maigizo yake kupitia runinga ya Independent Television ‘ITV’ kwa sasa alikuwa chini ya kundi la Ze Comedy ambalo hurusha michezo yake kupitia runinga ya East Africa Television (EATV).
Post a Comment