Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Nay wa mitego afunguka kwa mara ya kwanza .[CLICK PICTURE TO VIEW THENEWS]

KUFUATIA sintofahamu kati ya wapenzi wawili, Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’, ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na Siwema Edson juu ya mtoto wao mwenye umri wa miezi mitatu, mwanaume huyo amesema yupo tayari hata kwa http://www.hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/09/nay.jpgvipimo vya vinasaba (DNA) ili kuthibitisha kuwa Curtis ni mtoto wake wa damu. 


Msanii wa Bongo Fleva Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’.
Siwema ambaye Nay anadai kumfumania kitandani akiwa na mwanaume mwingine mjini Mwanza hivi karibuni, alisema Curtis si mtoto wa Nay, bali wa mwanaume mwingine ambaye hata hivyo hamtaji.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Nay alisema katika mambo yanayomshangaza na kumfedhehesha ni pamoja na ishu ya mzazi mwenzake kuropoka kuwa Curtis si mwanaye, kwani anaamini hayo ni maneno ya hasira na yeye ataendelea kumpenda mtoto wake.






Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’ na Siwema Edson wakiwa na mtoto wao.
“Ujue najiuliza sana maana ya kuongelea hili jambo mitandaoni, kusema Curtis siyo mwanangu, kiukweli ninamuacha aongee anavyotaka lakini nasisitiza kuwa ninampenda sana mwanangu,” alisema Nay wa Mitego.
“Niko tayari kupigana hadi tone la mwisho ili mwanangu aweze kuishi kwa amani na upendo na wala sioni tena kama kuna haja ya kuyapa nafasi maneno ya mtandaoni kwa sababu naamini Curtis ni mwanangu na nipo tayari hata kupima DNA nikibaini siyo wangu  nitajua la kufanya,” alisema Nay.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Daily News
Back To Top