Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

UGUNDUZI WA CHANJO MPYA WALETA MATUMAINI [CLICK PICTURE TO VIEW THE NEWS]


Baadhi ya dawa zinazotumika kupunguza makali ya virusi vya ukimwi.
Wananchi kutoka jiji la Dares salaam wametoa ya moyoni kufuatia kupata taarifa zinazoonesha kwamba huenda dawa ya kutibu ugonjwa sugu wa ukimwi ikapatikana.
Aidha, Wataalamu na Watafiti katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Temple, Marekani wamegundua dawa ya kuangamiza Virusi Vya Ukimwi (VVU) ambayo ni ya uhakika zaidi ukilinganisha na zilizowahi kupatikana katika tafiti za awali duniani.
Naye Dk Kamel Khalili amewaambia waandishi wa habari juzi mjini Philadelphia, Marekani kuwa tofauti na utafiti mwingine, wao wamegundua namna ya kukiondoa kirusi kilichoingia kwenye kinasaba (DNA) ndani ya CD4 na kukitoa nje na hatimaye kukiua.
Ameongeza kwamba ARV huangamiza VVU vilivyopo kwenye damu na kuendelea kuviacha hai vile ambavyo tayari vimeingia ndani ya CD4, hivyo kufanya virusi kuzuka upya pindi mwathirika anapoacha kutumia dawa.
Alisema ingawa tafiti nyingi hazijaonyesha matumaini waliotarajia ya kupata kinga na chanjo, bado juhudi zinaendelea ili kuhakikisha wanafikia mahali HIV inakuwa haina nafasi katika mwili wa mwanadamu.
Kwa Upande wa Salala Makambi kutoka chuo kikuu cha Tumaini jijini Dares salaam amesema kwamba ikiwa tiba ya ukimwi itapatikana basi dunia kwa ujumla itaokoa wananchi wengi walioteseka kwa miaka mingi sasa. Amesisitiza kwamba “cha msingi ni tusibiri ili tuweze kubaini kama ni kweli itafanikiwa kwa asilimia 100.”
Mwananchi mwingine ni Bi Sairice Fulko (Kinondoni)  amesema ripoti hiyo ya wataalamu ni habari njema kwa wananchi wote na dunia kwa ujumla.


author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Daily News
Back To Top